Header Ads

Kukithiri kwa Uchafu Geita, Wananchi walalamika.

WANANCHI wa mtaa wa mahakani kata ya Katoro Wilaya na Mkoa wa Geita wameiomba halmashauri ya mji mdogo wa katoro kuondoa uchafu uliopo katikati ya makazi yao kutokana na kuwa kero kwa muda mrefu.
Channel ten imetembelea eneo hilo na kujionea mafurushi ya uchafu yakiwa yamezagaa kwenye makazi ya watu suala ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu .
Wananchi wanaoishi maeneo hayo wakiwemo mama lishe wameiambia channel Ten kuwa pamoja na kutoa kiasi cha sh 1500 kila wiki kwa ajili ya kuzoa uchafu huo, lakini wanashangazwa kuona uchafu unakaa kwa muda mrefu hivyo kuomba wahusika kuundoa.
Mtendaji wa kata hiyo Aloyce Kamuri pamoja na mhudumu wa afya Estanael Riziki wamekiri kuwepo kwa uchafu huo na kwamba unazolewa ndani ya siku tatu na si kwamba huwa hauzolewi kama wanavyodai Wananchi
Mji wa Katoro uliyoko katika Wilaya ya Geita ni moja kati ya miji michafu kutokana na Halmashauri kutowajibika kuzoa uchafu unaokusanywa na Wananchi jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

No comments