Header Ads

ALIKIBA ADAI ALIANZA KUONYESHA ANAPENDA MUZIKI AKIWA NA SIKU 7.

Staa wa muziki Ali Kiba amesema wazazi wake walikiona kipaji chake cha muziki toka akiwa mchanga.
Akiongea na Chill na Sky  hivi karibuni,Kiba amesema alianza kucheza muziki akiwa na siku saba.

"Unajua mimi zamani kidogo wakati nazaliwa,nimeanza kucheza muziki nikiwa na siku saba.Nimeambiwa nilikuwa nikisikia muziki nacheza,mimi kitanda changu Baba yangu alininunulia kutoka Nairobi,kilikuwa kina redio,lazima waweke station ambayo inapiga muziki hapo ndio naweza kulala,ikizimwa nalia,"alisema Kiba.

Aliongeza,"Kwa hiyo nilikuwa mpenzi wa muziki tokea kipindi hicho na mpira ukaja baadae nikawa nacheza nyumbani,shuleni baadae nikawa vizuri kabisa,"

No comments