Header Ads

Jeshi la Polisi lawashikilia watu 33 wanaosadikika kuwa ni waharifu mkoani Geita

Jeshi la Polisi linawashikilia watu 33 wanaosadikika kuwa ni waharifu, wamekamatwa mkoani Geita katika operation maalumu ya kupunguza na hatimaye kutokomeza uhalifu mkoani Geita.

Akizungumzia tukio hilo na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Geita Lotson Mponjoli amesema miongoni mwa watuhumiwa hao wanne wamekamatwa kwa kosa la kukutwa na Bunduki moja ya kivita AK47 risasi 83 na bomu moja la kurushwa kwa mkono pia imekamata bunduki ya kienyeji aina ya Gobore, ambapo watu watano wamekamatwa kwa kosa la mauaji ya vikongwe na watu watatu walikamatwa kwa kosa la kuvunja na kuiba pia watu 17 walikamatwa wakipanga njama za kuiba katika mgodi mdogo wa Ibondo ambapo ilikamatwa kaboni  yenye thamani ya millioni miambili hamsini.

Aidha kamanda Mponjoli amesema vitu mbalimbali vimekamatwa katika operation hiyo ikiwemo Tv Radio Computer na samani mbalimbali za ndani.

Kamanda Mponjoli amesema operation hiyo ni endelevu na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha watu wanaishi kwa amani.


No comments