Header Ads

Wakazi wa Kijiji cha Nyamboge Wilaya ya Geita Wagomea Mradi wa Maji.

Wakazi wa Kijiji cha Nyamboge Wilayani Geita wamegoma kukabidhiwa mradi wa kisima cha Maji kilichofadhiliwa na Mradi wa World Bank kwa madai ya kuwa mradi huo uko chini ya kiwango na toka kisima hicho kijengwe januari mwaka huu hakitoi maji ya kuwatosheleza wakazi wa kijiji hicho.
Wakizungumza na Geita. Info wamesema wamepata mradi wa visima viwili vyenye thamani ya shilingi milioni 16 lakini toka mradi uanze kisima kimoja kimekuwa kinatoa maji kwa kusuasua na kingine hakitoi hali inayowafanya wananchi kutoona tija na mradi huo.
HABARI NA SALMA MRISHO(GEITA. INFO)

No comments