BAHEBE:MAMBO HAYAJILETI YENYEWE HUSABABISHWA KUTOKEA.
Mtangazaji na mmiliki wa PAULBAHEBE BLOG Paul B. William amewaasa vijana kufanya kazi na kutokutegemea serikali kwa kila kitu kwani serikali haimpi mtu pesa bali hutengeneza njia za mtu kumwezesha kupata pesa.
Akizungumzia maisha yake amesema kuwa yeye binafsi hakutegemea kama leo angekuja kuwa mtangazaji pamoja na kuwa na ndoto hiyo kwa muda mrefu,"nimepitia changamoto nyingi sana mpaka kufikia hapa nilipo leo japo ndoto yangu bado haijatimia,unajua kitu kikubwa ni kutokata tamaa pindi unapokumbana na changamoto.....maisha bila changamoto hayangekuwa na maana.....mambo hayajileti yenyewe bali husababishwa kutokea usikae kusubiri ajira kuna fursa nyingi tatizo letu vijana tunapenda mafanikio ya haraka jambo linalotufanya tushindwe kufikia malengo."Alisema wakati akiongea na PAUL BAHEBE BLOG.
Mtangazaji wa 88.9 STORM FM Paul William akipokea zawadi kutoka kwa Menaging Director wa STORM Modesta Mselewa wakati wa chakula cha jioni cha wafanyakazi wa STORM ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita GGM (village)
Post a Comment