Header Ads

STARS YAFUNGA KAMBI YA UTURUKI, SAFARI YA DAR YAANZA.


Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa kimefunga kambi yake hapa nchini Uturuki.


Stars imefunga kambi yake ya wiki moja kwenye mji mdogo wa Kartepe ambao uko milimani kabisa.

Kambi hiyo ilikuwa ni kujiandaa na mechi dhidi ya Nigeria Septemba 5 jijini Dar es Salaam kuwania kucheza Afcon.

Kikosi cha Stars chini ya Charles Boniface Mkwasa, kilimaliza mazoezi yake jana na leo wachezaji wake watasafiri kutoka Kartepe hadi mji mkubwa wa kibiashara wa Urutuki, Istanbul.


Stars itapande ndege ambayo itatumia saa nane kutoka hapa Istanbul hadi Dar es Salaam na kikosi hicho kitatua nyumbani Dar es Salaam, saa 9 alfajiri, usiku wa kuamkia Jumatano.

No comments