SERIKALI YAOMBWA KUTENGA MAENEO KWA WACHIMBAJI WADOGO GEITA.
Wakazi wa kijiji cha Mgusu Wilayani Geita katika mkoa wa Geita wameiomba serikali kuwapa Leseni wachimbaji wadogo wa eneo hilo,pamoja na kutenga eneo kwa ajili ya kuchimba kwani wamekuwa wakifukuzwa katika maeneo yao ambayo wengine wanasema kuwa wamekuwepo tangu miaka ya 1980 cha kushangaza leo wanaambiwa wavamizi hali ya kuwa mwekezaji mkuu(GGM) amewakuta wakifanya shughuli hiyo.
Ziara iliyofanywa na STORM FM pamoja na mwanaharakati/mshauri wa haki za binadamu kutoka umoja wa mataifa (UN) Bi.Chitra Massey,imebaini changamoto nyingi zilizopo katika eneo hilo zinazowakabili wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM),ikiwemo kero kubwa ya kutopatiwa maeneo kwa ajili ya uchimbaji pamoja na leseni.
Maji pia ni changamoto mojawapo katika kijiji hicho ambapo kina mama na watoto hulazimika kuamka mapema alfajiri kwenda kutafuta maji.
Bi.Massey akiwa pamoja na kina mama wanaofanya shughuli za kuponda mawe katika machimbo hayo ya Mgusu.
Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa kijiji cha mgusu akiwa katika picha ya pamoja na miongoni mwa wachimbaji hao pamoja na Mwakilishi wa umoja wa mataifa Bi. Chitra Massey.
Mwandishi wa habari wa kituo cha STORM FM Joel Maduka(kulia) akiwa na mmoja kati ya wachimbaji.
PICHA:JOEL MADUKA
Post a Comment