PLUIJM ANAAMINI YANGA ITAENDELEA KUTESA MSIMU UJAO.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ana imani kubwa na kikosi chake.
Pluijm amesema Yanga bado ina nafasi ya kufanya vizuri katika michuano yote ya mwakani.
“Michuano ya nyumbani na ya kimataifa, Yanga ina nafasi. Huenda wako wanaona kama kikosi chetu kina upungufu.
“Huenda ni baada ya kutolewa katika michuano ya Kagame. Lakini wanasahau kwamba tuna kikosi bora na ambacho hakijabadilishwa sana.
“Tunaendelea kuwaamini wachezaji wetu, tunaendelea kuyafanyia marekebisho makosa ambayo tumefanya au yalijitokeza ili kuwa boara zaidi,” alisema.
Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa Tanzania Bara, ubingwa walioubeba chini ya kocha huyo raia wa Uholanzi.
CHANZO SALLEH JEMBE
Post a Comment