MAANDALIZI UJIO WA DK. MAGUFULI YAENDELEA GEITA.
Mgombea kiti cha urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dk John Pombe Magufuli kesho jumatano anatarajiwa kuwasili mkoani Geita baada ya kumaliza mikutano yake katika miji ya Chato na Kagera jana.Maandalizi yanaendelea kupamba moto huku baadhi ya wananchi wakiongea na Paulbahebe blog wamekosoa vikali bango lililowekwa katika round about ya mjini Geita na kusema kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imekuwa ikiahidi ahadi lukuki ambazo utekelezaji wake umekuwa sifuri,wakitolea mfano bango lililowekwa katika round about hiyo wamesema badala ya kuboresha mazingira ya Geita kufanana na hadhi yake ya kutoa dhahabu kwa wingi,round about hiyo kwa miaka yote imekuwa ni moja kati ya round about nchini zenye kutia kinyaa ukilinganisha na hadhi ya Geita, ambapo leo kwa gharama nyingi kumewekwa bango kubwa la mgombea badala ya kufanya utaratibu wa kuipendezesha ifanane na mkoa.
Maandalizi ya ujio wa Dk. Magufuli katika uwanja wa kalangalala Geita mjini yakiendelea.
Ofisi ya CCM mkoa wa Geita
Post a Comment