Header Ads

KILA LA KHERI RAIS WETU JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Tanzania ikitegemea kumpata kiongozi mpya katika serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,kiongozi wa awamu ya tano,yapo mengi tunayojivunia,na kuyakumbuka katika uongozi wako.


Miundo mbinu,mawasiliano,pamoja na jitihada zako katika kupambana na ugonjwa hatari wa maralia bila kusahau usawa wa kijinsia pamoja na kupambana na vifo vya kina mama na watoto chini ya miaka mitano.



Majeshi yetu yote unayaacha katika hali nzuri yakiwa imara,binafsi nakumbuka kauli yako mwenyewe uliyowahi kusema kuwa "Tanzania tuko imara"





Kwa kiasi kikubwa umejitahidi kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na  mataifa makubwa na yaliyoendelea duniani japo wapo wanaobeza kuwa safari zilikuwa nyingi!lakini mimi najiuliza utawezaje kumshawishi mtu kuja kuwekeza kwako kama hujamfanya kwanza rafiki na kuwa karibu yake.

Mwenye macho haambiwi tazama,Tanzania imeendelea kuwa ni kisiwa cha amani na kuwa kimbilio la wageni na watu waliokosa tumaini-Tanzania inawakaribisha.!
Waswahili walisema "ukubwa jalala",nami nathubutu kusema uongozi ni kama jalala kila kitu kitatupiwa kwako,waziri kaharibu,mbunge kaharibu,mkurugenzi wa halmashauri na wengine hata balozi utasikia "yaani serikali ya Jakaya".
Hongera Mh. Rais kwa uvumilivu na ustahamilivu wako kwani umetukanwa,umebezwa na kusemwa lakini umeziba masikio na kutowasikiliza,hakika ningekuwa mimi nishakufa na presha.


PAUL BAHEBE ninakutakia maisha marefu urejeapo kijijini Msoga,kwani mimi naamini mamlaka yoyote inatoka kwa Mungu.

No comments