Header Ads

WAMILIKI WA BLOG NA WAHARIRI WAASWA.

1
Gasirigwa Sengiyumva kutoka MISA Tanzania, akitoa utangulizi juu ya mafunzo na kuwauliza wana bog na wahariri matarajio yao baada ya mafunzo hayo jana. 
2
Bw. James Malenga wa National Organization of Legal Assistance(NORA), akielezea juu ya sheria ya mitandao (ATI,RTI) na umuhimu wa kutoa taarifa wakati wa uchaguzi ,na kufafanua mwongozo wa uandishi na utangazaji kwa vyombo vya habari katika ukanda wa nchi za SADC(Role of Media in Elections)
3
Maxence Melo mkurugenzi wa – Jamii Media  aliyezungumzia juu ya sheria ya mitandao (Cybercrime) na sheria ya takwimu pamoja na matokeo yake wakati wa kuripoti habari wakati wa uchaguzi na umuhimu wa kutumia TEHAMA(ICT) pamoja na madhara yake. 
5678
4
Wamiliki wa Blog na wahariri wakifuatilia mafunzo hayo.

Na Gasirigwa G.S

Utoaji wa habari kwa usawa kwa kufuata sheria na taratibu,utoaji wa habari katika jamii ni miongoni mwa mambo yaliyozungumziwa katika mafunzo hayo ya siku moja kwa wamiliki wa bogs na wahariri jijini Dar es salaam jana.Wana blog na wahariri walielekezwa jinsi ya kutoa taarifa kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa ili kujiweka katika hali ya usalama, katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu october 25.
Mmoja wa wawezeshaji Bwana Maxence Melo alisema"wengi wenu hamuitilii maanani sheria hii ya makosa ya mitandao pamoja na mwongozo kwa vyombo vya habari iliyochapishwa katika gazeti la serikali mwezi wa sita mwaka huu,hii itawatia sana hatiani na wengi mtafungwa jela kama hamtakuwa makini.Wito wangu kwenu ni kuwa makini katika kazi zenu ndani ya sheria hii".
Mmoja wa wana blog na mwandishi wa habari za uchunguzi Danny Mbega alisema kuwa pamoja na kufanya kazi za habari kwa miongo kadhaa sasa lakini kuna vitu vingi alikuwa havielewi hadi leo.
Mafunzo hayo ambayo yalifanyika jijini Dar es salaam yaliwaleta pamoja wahariri kutoka vyombo tofauti 18 pamoja na wamiliki wa bloggs,ambapo pia mafunzo hayo yamedhaminiwa na CIPESA kutoka nchini Uganda.

IMETOLEWA :FULL SHANGWE BLOG NA KUTAFSIRIWA NA PAULBAHEBE

No comments