Header Ads

MGOMBEA UBUNGE GEITA KUPITIA CHADEMA AKANUSHA KUKIHAMA CHAMA.


                                                                   Rodgers Luhega

Aliyekuwa katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Geita ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Geita kupitia chama hicho Bwana Lodgers Luhega,leo amekanusha vikali habari zilizoenea kuwa amehama CHADEMA na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.


                                           Mr.& Mrs Rodgers Luhega wakiwa nyumbani.


Kauli hiyo imekuja baada ya habari za uvumi kuenea kwenye baadhi ya magazeti na mitandao ya kijamii,akizungumza na PAULBAHEBE BLOG Bwana Luhega alisema,


"Ni kwamba kuna uvumi lakini si tu uvumi ulikuwa unavuma lakini leo kuna magazeti yameandika kwamba mimi nimehama Chadema na kwamba ninagombea ubunge kupitia chama cha ACT. Ninakanusha vikali habari hii,mimi Rodgers Luhega bado ni mwanachama hai wa Chadema lakini pia sina kadi ya ACT wala sijawahi kujiunga na ACT wala sijawahi kushiriki kikao chochote cha ACT"Amesema Rodgers.

Lakini Paul Bahebe ikaona ni vema ikautafuta pia uongozi wa ACT mkoa wa Geita ili kulizungumzia suala hilo,Ikongoro Emmanuel ni katibu wa chama cha ACT mkoa wa Geita ambaye kwa kifupi aliongea haya yafuatayo:-
"Sisi bado hatujampokea rasmi Rodgers kuwa mwanachama wetu....ila tunamkaribisha kama yupo tayari aje aungane na sisi katika kupigania haki na uzalendo........."

                                        Katibu wa ACT mkoa Geita Bw.Ikongoro Emmanuel


No comments