MAJINA YA WALIOTEULIWA UBUNGE, UWAKILISHI NA VITI MAALUM CCM YATANGAZWA RASMI.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020 ya CCM wakati wa kufunga kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kumaliza zoezi la kupitisha majina ya wagombea Ubunge na Uwakilishi mjini Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipitia orodha ya majina ya waliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge na Uwakilishi,kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda.
MNEC wa Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akipitia kitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kitakachotumika kwa mwaka 2015-2020.
Dk. Salim Ahmed Salim akipitia majina ya walioteuliwa wakatia wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambapo alitaja majina ya walioteuliwa na zile sehemu chache ambazo uchaguzi utarudiwa na sehemu zingine kufanyiwa uhakiki upya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha halmashauri kuu ya CCM (NEC) katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ndugu NAPE NNAUYE amesema vikao vimekuwa virefu lakini vyenye mafanikio makubwa nakusema wagombea wote waliochukua fomu ni elfu 2721
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipitia orodha ya majina ya waliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge na Uwakilishi,kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda.
MNEC wa Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akipitia kitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kitakachotumika kwa mwaka 2015-2020.
Dk. Salim Ahmed Salim akipitia majina ya walioteuliwa wakatia wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambapo alitaja majina ya walioteuliwa na zile sehemu chache ambazo uchaguzi utarudiwa na sehemu zingine kufanyiwa uhakiki upya.
CHAMA Cha Mapinduzi kimemaliza vikao vyake vya juu vya kupitia uteuzi wa wagombea ubunge na uwakilishi katika majimbo yote nchini huku majimbo 11 kati ya 240 yaliyopo nchini yakisubiri uamuzi wake kutolewa Agosti 17 na Kamati Kuu maalum ya CCM.
Post a Comment