Header Ads

ZIARA YA RAIS OBAMA NCHINI KENYA.

OBAMA ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA SITA WA KIMATAIFA KUHUSU UJASIRIAMALI KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA MJINI NAIROBI.
11.10am:Mermorial Park
Obama na Uhuru sasa waelekea katika eneo la shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 jijini Nairobi
10.55am:
Obama na Uhuru
Obama amaliza hotuba yake
10.50am:BBC hewani moja kwa moja
Obama
Runinga ya BBC inapeperusha moja kwa moja kongamano hilo hewani
10.48am:Mpesa
Kenya inaongoza katika teknolojia za kibiashara.Kwa mfano utumizi wa Mpesa-ni vyema kwamba teknolojia hiyo ilianza hapa Kenya
10.41am:Rais Obama
Rais Obama
Rais Obama awasalimia wakenya kwa neno 'niaje' na kusema kuwa familia yake inatoka nchini kenya.
Lengo la mkutano huu aliouzindua miaka mitano iliopita mjini Washington ni kuwapiga jeki wafanyibiashara duniani.
Amesema kuwa kuna umuhimu wa kukabiliana na ufisadi ili biashara kushamiri.
10.35am:Uhuru Kenyatta
Kenya ilikumbwa na chanagamoto chungu nzima ikiwemo majanga lakini imesimama imara na kusonga mbele.
Bara la Afrika haliwezi kutegemea mataifa ya magharibi .
Taifa la kenya ni chimbuko la makabila tofauti.
10.15am:Mkutano waanza
Mkutano wa wajasiriamali umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano
10.00am:Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta
Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa tayari umewasili katika eneo la mkutano wa wajisiriamali unaotarajiwa kufunguliwa na raia wa marekani Barrack Obama
09.45am:Waandishi
Waandishi habari
Waandishi
Waandishi wa habari wakijiandaa kuliangazia kongamano la kibiashara la wajasiriamali katika eneo la Gigiri jini Nairobi.Vifaa vya waandishi hao vimepekuliwa na maafisa wa usalama wa Marekani.
09.00am:Ndege Nairobi
Ndege za kijeshi
Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kuzunguka katika anga ya jiji la Nairobi kuimarisha usalama.
08.30am:Barabara za Jijini Nairobi:
barabara
Barabara nyingi za mji wa Nairobi zimeonekana kuwa bila watu na magari kufuatia kuwasili kwa rais Obama.Mapema leo maafisa wa polisi walionekana katika barabara zinazoelekea katika eneo la Gigiri ambapo rais Obama atafungua rasmi kongamano la kibiashara.
08.20am:Obama na familia yake
Sara Obama,Barrack Obama na Daktari Auma
Mama Sarah Obama,Rais Obama na dadaake Daktari Auma Obama wakijumuika katika chakula cha jioni katika hoteli moja jijini Nairobi.

No comments