Header Ads

WAZIRI MKUU WA UGIRIKI AZIDI KUBANWA.

Alexis Tsipras,Waziri Mkuu wa Ugiriki
Waziri mkuu wa ugiriki Alexis Tsipras anazidi kukabiliwa na upinzani huko Athens kwa hatua mpya na kali za malipo alizokubali kuzitambulisha kutokana na masharti mapya ya kuokoa kuporomoka kwa uchumi.
Waziri wa ulinzi wa Ugirik Panos Kammenos ambaye anaongoza chama kidogo katika muungano wa serikali ya kitaifa alielezea mpango huo kama mapinduzi ya serikali. Habari kutoka kwenye chama chake mwenyewe zinasema mkataba uliowekwa ni wa kuifedhehesha Ugiriki. Mpango huo unataka bunge la ugiriki kupitisha ongezeko la kodi, kupunguza mafao, na kufanya mabadiliko ya sheria ya ajira ifikapo Jumatano. Waziri wa kazi wa Ugiriki, Panos Skourletis , alionya kuwa kuungwa mkono kwa hoja hiyo bungeni hakutakuwa rahisi . Chama cha watumishi wa umma wametangaza saa ishirini na nne wa mgomo ifkapo jumatano kuonesha kutokunga mpango huo.BBC

No comments