Header Ads

WAMAASAI WATAKAOMTUMBUIZA OBAMA.

Kundi la Olalang
Huku usalama ukiwazuia maelfu ya mashabiki wa rais wa Marekani kukutana naye ama hata kuhudhuria kongamano atakalohutubia katika ziara yake ya siku tatu mjini Nairobi Kenya, kundi la waimbaji kutoka jamii ya kimaasai imepata fursa ya kipekee.
Waimbaji hao wametunukiwa jukumu la kumtumbuiza rais Obama.
Kundi hilo la Olalang ndilo litakalomburudisha rais Obama atakapozuru Kenya leo.
Kundi hilo la Kimaasai kutoka mji wa Maasai Mara nchini Kenya limeandaa nyimbo na densi za kimaasai tayari kabisa kukonga moyo wa kiongozi mwenye nguvu zaidi duniani.
Kundi hilo linalowajumuisha wanaume na wanawake kutoka jamii ya maasai limekuwa likifanya mazoezi kwa zaidi ya miezi mitatu tangu lilipoarifiwa kuwa litamtumbuiza rais Obama.
Wanachama wa kundi hili wamevalia sare na mapambo ya kimaasai.
Wanachama wa kundi hili wamevalia sare na mapambo ya kimaasai.
Tabasamu yao inaoana na rangi nyekundu ambayo inatawala taswira ya sare yao rasmi.
Kila mmoja akiwa ni mchangamfu kutokana na burudani kali anayotarajiwa kutoka kwao.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Gideon ole kitare, anasema kuwa wanafurahia kuchaguliwa kumpokea mgeni wa hadhi ya Rais Obama.
‘Hii ni mara yetu ya kwanza kuwa katika ngazi ya kimataifa na tunatarajia kuwa itakuwa ni fursa kubwa kuonekana na wageni kutoka nchi za nje na hata kualikwa kuandaa burudani nje ya nchi.
Hata hivyo, kundi hili ni la densi maalum kwa Rais Obama kinyume na densi za kawaida.
James Ole Kar Kar, mmoja wa waimbaji wa kundi hili, anasema kuwa wamejumuisha nyimbo na densi maalum za kimaasai kwa sababu ya rais Obama.
‘’Tumemuandalia wimbo unaoitwa ''Orkonti'' ambao ni wimbo wa kumkaribisha shujaa kama Rais Obama.’’
‘’Wimbo huo ni wa kumpa nguvu shujaa ili aweze kuwa na uwezo wa kufanya mambo muhimu.’’ Aliongeza
Sylvia Lesaloi,anasema watampokea rais Obama kama 'mtoto anayerejea nyumbani '
Kwa upande wake, Sylvia Lesaloi, mmoja wa viongozi wa kundi hili, anasema kuwa yeye pamoja na kina mama wenzake katika kundi hilo, watampokea Rais Obama kama mtoto anayerejea nyumbani baada ya kuondoka kwa kipindi kirefu.
‘’Rais Obama ni mtoto wetu, tunafurahi ametutembelea safari hii na pia tungependa awe akitutembelea hata atakapomaliza muhula wake kama rais wa Marekani.''
Aidha Bi. Sylvia ana ujumbe moja tu kwa Rais Obama.
'' iwapo tutapata fursa ya kuwasilisha ombi kwa Rais Obama, Tutamuomba atusaidie kuhifadhi msitu wa Mau ambao unatishiwa na unyakuzi na uharibifu wa kimazingira.''
''Tuanomba atausaidie ili tuweze kuulinda msitu huo wa Mau’’.
Msitu wa Mau ni msitu mkubwa wa kiasili na ambao ndio chanzo cha mito mingi inayotiririka kupitia mbuga kuu ya wanyama ya Maasai Mara na pia mito inayotiririka hadi kwenye ziwa Victoria.
Hata hivyo katika miaka ya hivi punde viongozi wa kuu katika serikali zilizopita nchini Kenya walinyakua vipande vikubwa vya msitu na kukata miti.
Wamaasai watakaomtumbuiza Obama wakiwa na mwandishi wetu Abdi Noor
Athari yake imekuwa kupunguka kwa kiwango cha mvua katika maeneo karibu na msitu huo.
Eneo la Maasai Mara, makao ya kundi hili, ni eneo alilozuru rais Obama alipowasili nchini Kenya mara ya mwisho.
Eneo hilo ni mojawapo ya maeneo yanayowavutia watalii wengi wa kigeni nchini Kenya.
Densi na nyimbo za kimasaai zimekuwa na mvuto mkubwa kwa watalii nchini Kenya lakini wanachama wa kundi hili wanasema kuwa Obama sio mtalii wa kawaida ni shujaa wa hapa nchini Kenya.BBC

No comments