TUKIO LA MLINZI KUUAWA NYARUGUSU GEITA RPC ATHIBITISHA.
MTU MMOJA ANAYEJULIKANA KWA JINA LA LUKASI
CHUMA MWENYE UMRI MIAKA 27 MLINZI WA
LAMPASI SECURITY AMEUWAWA KWA KUCHOMWA
NA KITU CHA NCHA KALI KICHWANI NA WATU WASIO JULIKANA WAKATI ALIPOKUWA KATIKA
LINDO KWENYE HOTEL YA NELLYS ILIYOPO KATA YA NYARUGUSU.
KWA UPANDE WAKE MENEJA WA NELLY HOTEL,BW ERICK ELIAS
WAKATI AKIZUNGUMZA NA STORM FM ,AMESEMA KUWA TUKIO HILO LIMEMKUTA AKIWA AMELALA
NYUMBANI BAADA YA KUPATA TAARIFA KWA MTU
WA MAPOKEZI KUWA MLINZI AMEPOTEZA
MAISHA.
AKITHIBITISHA TUKIO HILO KAMANDA WA MKOA WA
GEITA,JOSEPH KONYO, AMESEMA KUWA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI WA
KUWEZA KUBAINI NI NANI AMBAE AMEHUSIKA NA TUKIO HILO.
Post a Comment