Morocco: Ugaidi unatofautiana na dini ya Kiislamu.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Morocco amekosoa mienendo ya makundi ya kigaidi yanayovihusisha vitendo vya kigaidi na dini ya Kiislamu.
Ahmed Toufiq aliyasema hayo hapo jana mjini Dakar, Senegal ambako kunafanyika kongamano linalojadili masuala ya Uislamu na amani. Sanjari na kulaani mienendo ya magaidi wanaotenda jinai kwa kutumia jina la Uislamu, alisema kuwa makundi hayo yanajaribu kuionyesha dini hii ya mbinguni kuwa ni dini ya vita pekee.
Mmoja wa viongozi wanaoshiriki katika kongamano hilo, Mamdo Lamin, alihutubia kikao hicho kwa kusema kuwa, wale wanaotekeleza jinai kwa kutumia jina la Uislamu huko nchini Nigeria, Syria, Iraq na maeneo mengine ya dunia, hawana elimu hata kidogo na misingi ya dini ya Kiislamu.
Amesema kuwa moja ya malengo makuu ya kongamano hilo la Uislamu na amani, ni kuitambulisha sura halisi ya dini hii ya Kiislamu na kuusafisha kutokana na vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na watu wachache wanaotumiwa na madola ya Magharibi ili kuichafua dini hii ya amani.
Kongamano hilo limeitishwa na serikali za Senegal na Morocco na linahudhuriwa na karibu wasomi na wataalamu wa dini wapatao 500 kutoka nchi 20 za dunia.IRAN RADIO
Post a Comment