BIBI AMUANDALIA OBAMA UGALI, MBOGA ZA KIENYEJI.
Mwandishi wetu
LICHA ya Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi kusisitiza kuwa Rais Barack Obama hatatembelea Kijiji cha K’Ogelo, alikozaliwa baba yake mzazi, bibi yake, Mama Sarah Obama amesema atamuandalia chakula kizuri cha kiasili ukiwamo ugali na mboga za majani za kienyeji.
Bibi huyo, mke wa tatu wa babu yake Obama, aliwaambia waandishi kuwa anategemea kukutana na mjukuu wake huyo kijijini K’Ogelo wakati wa ziara hiyo kwa vile anampenda na angefurahi kutembelea kaburi la baba yake mzazi.
“Hii ndio boma ya baba yake, sasa mimi naweza kusema nini, hakuna maneno mimi iko nayo, wewe ulikuwa nataka mimi nachinja nini? Yeye nakula hata Omena hata mboga, chakula ile mimi nakula ndio yeye nakula,” mama Sarah aliiambia BBC.
Kaburi la baba yake Rais Obama limekarabatiwa kuelekea ziara hiyo licha ya Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec kusisitiza kuwa kiongozi huyo mwenye mvuto hatazuru K’Ogelo.
Post a Comment