Header Ads

BIASHARA YA NGONO YASHAMIRI MKOANI DODOMA.

Wakati vikao vya kumpata mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) vinaendelea mjini Dodoma,biashara ya ngono nayo inazidi kushamiri katika baadhi ya kumbi za starehe kama Club Maisha,Club Laaziz na kumbi zingine.

Eneo maarufu la Chako ni chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha akina dada wamekuwa wakijazana kutafuta wateja huku wengine wakisimama kwenye taa za kuongozea magari kwa lengo la kupata wateja kwenye magari.

Mmoja kati ya wadada hao alisema kuwa ana siku tatu akiwa Dodoma na tayari amekusanya zaidi ya Tshs.700,000,huku akiwatumia madalali ambao huwaunganisha kwa wateja "wazito"(wenye fedha) kwa ujira maalum.

No comments