BENDERA YA KIKOLONI KUONDOLEWA S.CAROLINA.
Maseneta wa jimbo la South Carolina nchini Marekani wamepitisha sheria inayoharamisha kupeperushwa benderea ya kikaburu iliyotumika nchini humo wakati wa utumwa.
Hatua hii inafuatia kisa cha mwanamume aliyewapiga risasi na kuwaua waumini wa kikristu weusi katika kanisa moja mwezi Juni.
Mwanamume huyo Dylann Roof 21, alionekana katika baadhi ya picha zake akipeperusha bendera hiyo.
Kwa miaka mingi bendera hiyo imechukuliwa kuwa ishara ya ubaguzi wa rangi na udunishwaji wa watu wa rangi nyeusi na vizazi vyao.
Sasa sheria hiyo inasubiriwa kuidhinishwa na bunge la waakilishi.
Hata hivyo sharti itekeleze sharti la kupigiwa kura na thuluthi mbili ya wabunge kabla haijatiwa sahihi na kuidhinishwa na gavana kuwa sheria.
Wajumbe kadhaa walioipigia kura kauli hiyo walisema kuwa walivutiwa na msamaha uliodhihirika kutoka kwa jamaa ya waliofiwa baada ya shambulizi hilo lililovutia hisia nyingi.
Roof aliishambulia kanisa la kihistoria la Emanuel AME juni 17 na kuwaua watu 9 akikusudia kuanzisha uhasama baina ya wazungu na watu weusi.BBC
Post a Comment