WAKRISTO WATAKIWA KUMUOMBA MUNGU ALIEPUSHE TAIFA NA MATUKIO YA UBAGUZI
Kiongozi wa kanisa katoliki nchini Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amewataka wakristo kote nchni kumuomba mungu aliepushe taifa na matukio ya ubaguzi, vita, ugaidi na mauaji yanayotokea Duniani ikiwemo mauaji ya kikatili ya wanafunzi waumini wa kikristo yaliyotokea katika chuo kikuu cha Garisa nchini Kenya.
Akizungumza katika ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa shirikisho la kwaya katoliki nchni, Kadinali Pengo pia amewataka wakristo nchini kumuomba mungu asafishe hali iliyojitokeza nchini Kenya na kuwataka kuwawajasiri na kubaki katika misimamo ya imaniya kikristo kwa kutamka ukweli iwapo hali hiyo italazika kujitokeza.
Aidha kuhusu katiba inayopendekezwa,Padinali Pengo amesema kama kiongozi wa Dini hawezi kurudia au kubadilisha kauli aliyokwisha itoa kwa wananchi,kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha ugomvi ambapo amewataka waumini wa kanisa katoliki kusambaza kauli hiyo kote nchni.
Awali kiongozi wa kanisa katoliki nchini Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ametaka wananchi waachiwe wasome katiba inayopendekezwa na kufanya maamuzi wenyewe. habari na ITV
Post a Comment