PAKA ALIYEHUDUMU KAMA MKUU WA KITUO CHA RELI.
Paka mmoja wa Japani ambaye alipata umaarufu alipofanywa kuwa mkuu wa kituo cha reli, amefariki, na waombolezaji wengi wamejitokeza.
Wakuu na washabiki walihudhuria mazishi ya paka huyo, katika kituo cha reli, ambako alitumika.
Paka huyo aliyejulikana kwa jina ''Tama'' ambaye alipatikana akiranda randa katika kituo cha reli cha Kishi miaka minane iliyopita kabla yake kutawazwa kuwa meneja wa kituo hicho,
aliaga dunia majuzi kutokana na umri wake mkubwa wa miaka 16.
Tama aliishi katika kituo hicho akiwa amevalia sare rasmi ya afisa mkuu wa kituo cha reli na kuibuka kuwa kivutio kikubwa cha watalii.
Alivishwa kofia na kikoti maalumu alichoshonewa.
Viongozi na wananchi wa matabaka mbalimbali walimmiminia sifa paka huyo hasa wakisema kuwa ndiye aliyefufua kituo hicho cha reli.
Rais wa shirika la reli ya umeme la Wakayama Japan , bwana Mitsunobu Kojima, alimsifu Tama kwa kufufua uchumi katika eneo zima la Wakayama.
'' Bi Tama, japo umetuacha ninakupa heshima na kuanzia leo utasalia kuwa mkuu wa kituo hich cha reli milele''alisema Kojima
tangazo hilo lilishangiliwa na waombolezaji waliofika katika maziko hayo.
Pengo lililoachwa na kifo cha bi Tama tayari limejazwa na paka mwengine mpya ambaye kwa sasa hajapewa heshima za kuwa mkuu wa kituo hicho.
Gavana wa kanda hiyo ya Wakayama , Yoshinobu Nisaka, amewashauri wadogo wake wamtunze mrithi wa Tama na vilevile wamfunze kazi.
''itakuwa bora sote tukichukua jukumu la kuendeleza utamaduni wa kihistoria ulioachwa na bi Tama''alisema gavana Nisaka.
Tama kama paka huyo alivyofahamika alilelewa na wafanyikazi wa reli katika kituo hicho cha Kishi.
Hata hivyo maisha yake yalibadilika shirika la reli lilipowafuta kazi wafanyikazi wote katika kituo hicho n hivyo akasalia humo asijue pa kwenda.
Tama baadaye alitambuliwa na wakuu wa shirika hilo na hivyo akatawazwa kuwa mkuu wa kituo hicho.
Umaarufu wake uliibua mtindo mpya wa mavazi ya paka,biashara ambayo hadi sasa inanogo katika eneo hilo la Kishi na Japan kwa jumla.
Aidha watalii walibadili safari zao na kupitia katika kituo hicho cha reli ilikujionea wenyewe ''afisa huyo mkuu'' akihudumia abiria.
Maajabu ya ulimwengu!
Post a Comment